-KATIKA IMANI ZA UISLAM:Ni kuamini kuwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni ni katika makadirio ya Allah na tayari kimeshaandikwa kabla ya kutokea,pamoja na kuwa mwanadamu ameamrishwa kufanya mambo yatakayosababisha(utokeaji wa kitu hicho)na ndiye mfanyaji wa kitendo na anastahiki kuulizwa kutokana na mambo anayoyafanya na kila ambacho
kitafatana na matendo yake duniani na akhera,na haifai kuacha kitendo kwa kutoa hoja ya makadirio.Itikadi hii itakufanya uishi kwa utulivu.
6-Uislamu:Unaamrisha kufanya uadilifu,wema,kuunga undugu,kujizuia kutokana na machafu,ukweli…na sifa zote zilizo nzuri,na unakataza dhulma,zinaa,wizi,uadui kwa watu,kuua nafsi iliyohifadhika,uongo,kujifaharisha…na sifa zote zilizo mbaya,na baadhi ya makosa ambayo yanapatikana kwa baadhi ya watu ambayo hayalingani na uislamu hayo yote yanarudi kwa watendaji wa matendo hayo na uislamu uko mbali na makosa hayo.