NYUMBANI
MAKTABA
_RelatedSite
KUHUSU SISI
WASILIANA NASI
_IyHAqoaspsitu
JINA
BARUA PEPE

_LATEST_BOOK
MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU UISLAMU
Hisn Al-Muslim
SALA
 
NAMNA YA KUSALI
 
1-Uelekee Qibla(Al-kaabah)na usema:( )Allahu Akbar,(maana yake Allah ni mkubwa)huku ukiwa umenyanyua mikono yako usawa wa masikio kisha utaweka mkono wako wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika kifua chako,kisha utasoma surat-Fatiha:
    (Unaanza na dua ya kufungulia sala nayo:
.
Sub-haanaka Allahumma wabihamdika watabaaraka smuka wataa'laa jadduka walaa ilaaha gh'ayruka.
Maana yake:
Utakasifu na sifa njema ni miliki yako ewe Allah na jina lako limetukuka na utukufu wako uko juu na hapana muabudiwa wa haki ila wewe.
                                                                                                       
(1) (2) (3) (4) (5)
(6) (7)
Maana yake:
Nataka hifadhi kwa Allah kutokana na shetani aliyefukuzwa kutoka katika rehema za Allah.
(1)Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
(2)Kila sifa njema anastahiki Allah Mola wa viumbe wote(3)Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu(4)Mfalme wa siku ya malipo(5)Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekutaka msaada(6)Tuongoze njia iliyonyooka(7)Njia ya wale uliowaneemesha,sio ya walioghadhibikiwa na waliopotea.
                                        Amiin(Allah ikubali dua)
Kisha baada ya hapo unaamrishwa kusoma sura yoyote iliyo nyepesi katika Qur-ani kama vile suratil-Ikhlas,utasema:
 
)1(  (2)   (3)       (4)
 
Maana yake:
(1)Sema!(ewe Muhammad)Huyo Allah ni mmoja(2)Allah ndiye wa kukusudiwa(katika kila jambo)(3)Hakuzaa wala hakuzaliwa(4)Na hakuna yoyote aliyefanana naye.
2-Kisha utasema: (Allahu Akbar),utarukuu(yaani utainama hali ya kuweka mikono yako katika magoti)na utasema:
( ) Sub-haana Rabiyal-A’adhwiym
(yaani:Utakasifu ni wa Mola wangu Mtukufu)
na ni vizuri kulikariri(mara nyingi).
3-Kisha utanyanyuka kutoka katika rukuu na kusema) )Sami’a Allahu liman hamidah
(yaani:Allah amemsikia yule ambaye amemshukuru).
4-Kisha utaporomoka na kusujudu,na ndani ya sijida yako utasema:
( ) Sub-haana Rabiyal A’alaa
(yaani :Utakasifu ni wa Mola wangu aliye juu)
ni vizuri kuikariri mara nyingi.
5-Kisha utasema;( )Allahu Akbar,utakaa kitako na kusema:
 ( ) Rabbiy ghfir liy(yaani:Ewe Mola wangu nisamehe)
Utalikariri mara nyingi.
6-Kisha utasema: ))Allahu Akbar,na utasujudu na ndani ya sijida yako utasema   )) Subhaana Rabbiyal A’alaa.
Utalikariri mara nyingi.
7-Kisha utasema:( )Allahu Akbar,na utasimama ili kuleta rakaa ya pili,na utafanya katika rakaa yako ya pili kwa mfano kama huu uliotangulia katika rakaa ya kwanza.
8-Utakapomaliza kusujudu katika rakaa yako ya pili utasema:( )Allahu Akbar,
baada ya hapo utakaa kitako kwa ajili ya kusoma tashahudi ya kwanza nayo ni:
 
Attahiyyatu lillahi waswalawatu watwayyibaatu Assalamu a’layka Ayyuhannabiyy warahmatullahi wabarakaatuhu,Assalamu a’layna wa a’laa I’baadillahi swaalihiyna,Ash-hadu Allaa ilaha illallah wa-ash-hadu Anna Muhammada A’bduhu warasuuluhu,
Maana yake:
(Maamkizi,rehema na yaliyo mazuri ni miliki ya Allah,amani,rehema za Allah na baraka zake ziwe juu yako ewe Mtume(s.a.w)amani ziwe juu yetu na juu ya waja wa Allah walio wema,nashuhudia ya kuwa hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na nashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wa Allah na ni Mtume wake.
9-Kama sala unayosali ni ya rakaa mbili utaikamilisha kwa kusoma tashahudi ya mwisho mpangilio wake unakuja katika kipengele kifuatacho,kisha utatoa salamu,na kama sala ni zaidi ya rakaa mbili utalazimika kusimama baada ya kumaliza kusoma tashahudi ya kwanza na utafanya matendo yaleyale uliyofanya katika hatua zilizotangulia.
10-Mwisho wa sala utasema:) ) Allahu Akbar,kisha utakaa kitako na kusoma tashahudi ya kwanza na utafatishia kusoma tashahudi ya mwisho nayo ni:
 
.
.
 
Allahumma swalli A’alaa Muhammadi wa A’alaa Aali Muhammadi kama swalayta A’alaa Ibrahima wa A’laa Aali Ibrahima innaka hamiydun Majiidu,
Allahumma Baariki A’alaa Muhammadi wa A’laa Aali Muhammadi kama barakta A’laa Ibrahima wa A’laa Aali Ibrahima Innaka Hamiydun Majiydu.
Maana yake:
(Ewe Allah mrehemu Muhammad na jamaa wa Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na jamaa wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye kushukuriwa na Mtukufu.
Ewe Allah mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammadi kama ulivyombariki Ibrahim na jamaa wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye kushukuriwa na Mtukufu.
11-Baada ya tashuhudi ya mwisho utasema:
     .
)
 
Allahumma rabbanaa Aatinaa fiy Duniya hasanatan wafil-Aakhirat hasanatan waqinaa A’dhaaba nnaar,Allahumma Inniy A’udhubika min A’dhaabi jahannama wamin A’dhaabil-qabri,wamin fitinatil-mahyaa wamamaat wamin fitinatil-masiyh dajjaal.
 
Maana yake:
Ewe Mola wetu tupe mazuri duniani na akhera na utukinge kutokana na adhabu ya moto.
Ewe Mola hakika mimi ninataka hifadhi kwako kutokana na adhabu ya Jahannam na kutokana na adhabu ya kaburi,na( ninataka hifadhi)kutokana na fitina za uhai na za umauti,na kutokana na fitina za Masihil-Dajjaal.
12-Baada ya hapo geuka upande wako wa kulia useme
(Assalaamualayku warahmatuyllah)                                                        
kisha geuka upande wa kushoto na sema:
(assalaamualaykum warahmatullah                                                      
Maana yake: Amani na rehema za Allah ziwe juu yenu.
KURASA KUU
UISLAM NI
TOHARA
SALA
SALA TANO
Question And Answer
 
LUGHA
العربية Arabic
انجليزي english
صيني china
كينى Kenya
نيبالي nip
ألماني grmany
تجالوج TAGALOG
بيساو Bisaya
كلقان Kalagan
هندى hindi
تاميلي tamil
السواسيلندية Swaziland
بنقالية bangal
فيتنامي vitnam
هوسا Hausa
اليابانية Japan
تركي torke
روسي rose
اسباني Español
كوري cory
أندونيسيا indonesia
لينغالا-كونغو LINGALA
رواندا raounda
برمجة و تطوير الموقع اكساء لتكنولوجيا المعلومات